September 5, 2019


Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amegoma kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbao wakati timu hiyo itakapokuwa kambini jijini Mwanza.

Yanga ambayo itaweka kambi jijini humo kujiandaa na mchezo wa kimataifa Septemba 14 jijini Dar, dhidi ya Zesco kutoka Zambia, ilitakiwa icheze mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbao FC.

Zahera ameliambia Championi Jumatano, kuwa sababu ambazo zimempelekea kukataa kucheza mchezo huo ni kutokana na Mbao kuwa miongoni mwa timu zinazocheza ligi kuu ambazo mara nyingi hukamia timu kubwa pindi zinapokutana.

“Mbao ni timu inayoshiriki ligi kuu, kama unavyofahamu pindi timu kama Mbao inapocheza na timu kubwa hukamia kitu ambacho si kizuri kwani kinaweza kutusababishia majeruhi katika timu yetu.

“Tulipoweka kambi Kilimanjaro tulicheza na Polisi Tanzania, walitukamia sana bila kujali afya yetu, endapo tutacheza na Mbao FC yanaweza yakajitokeza yale ya Polisi Tanzania kitu ambacho ni hatari kwa afya yetu,”alisema Zahera na kuongeza kwamba anataka kucheza na timu za madaraja ya chini.

4 COMMENTS:

  1. Ukitaka kuuwa Simba, usijipime Kwa kuuwa ngedere

    ReplyDelete
  2. Hapo hakuna kocha ni magumashi tupu.

    ReplyDelete
  3. yuko sahihi mechi ya kufungua ligi simba na azam,azam walichezakwakukamia na rafu nyingi wakati simba ilikuwa na mchezo unaofuata

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dah nimerudia video clipsbhii mechi Azam alicheza kwa ubabe sana na faulo aliyochezewa Bocco haikuwa ya ungwana na imeicost sana Simba

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic