September 5, 2019


Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ametamba kwamba atafanya njia yoyote kuhakikisha kwamba anafikia rekodi ya kocha wa Simba, Patrick Aussems kwa kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Zahera ana mtihani wa kufikia rekodi ya Aussems ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo watavaana na Zesco inayofundishwa na aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo, George Lwandamina.

Timu hizo zitapambana Septemba 14 katika mechi ya kwanza itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Zahera amesema kuwa anaelewa juu ya uzito uliopo mbele ya Zesco wa kuwafunga na kuwatoa lakini anaendelea kujipanga na kuendelea kusuka mikakati yake kuona anashinda na kuweka rekodi ya kutinga hatua ya makundi ya kombe hilo kubwa kwa upande wa klabu barani Afrika.

“Naelewa ugumu halisi ambao upo mbele yetu wa kushinda na kutinga kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwaondoa Zesco.

"Najua kabisa kwamba itakuwa mechi ngumu kwetu na lazima tuongeze juhudi ili tushinde. “Lakini tunataka kuweka rekodi mpya kwa kushinda mechi hiyo.

"Nahitaji kuona kwamba tunafika katika hatua ya makundi ya kombe hilo na tutalitimiza hilo kutokana na namna tunavyojiandaa hadi sasa, nina uhakika mkubwa wa kushinda katika mchezo huo mbele ya Zesco,” alisema Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic