ZANA AWASHANGAA SIMBA
Beki wa zamani wa Simba, Zana Coulibaly ameibuka na kusema kuwa hakutarajia kuona Simba ikiondolewa mapema katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Coulibaly alijiunga na Simba katika kipindi cha dirisha dogo msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili lakini hakuweza kudumu katika timu hiyo kufuatia kusitishiwa mkataba wake kisha kujiunga na AS Vita ya DR Congo ambayo inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Coulibaly alisema kuwa hakutarajia kuona Simba ikiondolewa mapema katika michuano hiyo kutokana na aina ya kikosi walichosajili pamoja na uwekezaji mkubwa
uliopo kwenye timu hiyo.
“Kwangu nashukuru Mungu naendelea vizuri lakini sijui nini kimewapata Simba katika Ligi ya Mabingwa msimu huu, naona wametolewa mapema na haikuwa mipango yao kutokana na kocha alivyokuwa akieleza.
“Siwezi kuwalaumu kwa kuwa sijui nini kimewakuta kwa sababu kama usajili wao waliweza kufanya kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi na ukiangalia Simba msimu uliopita ilifanya kitu kikubwa katika soka la Tanzania,” alisema Coulibaly aliyekuwa akicheza nafasi ya beki wa kulia.
0 COMMENTS:
Post a Comment