October 25, 2019


MTENDAJI Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amefunga mjadala wa wachezaji wa kikosi hicho ambao awali ilidaiwa ni watovu wa nidhamu hali iliyofanywa kuwekwa pembeni.

Wachezaji hao ni Jonas Mkude, Clatous Chama, Erasto Nyoni na Gadiel Michael ambapo inaelezwa kuwa, walifanya vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Simba ikijiandaa kwenda Kanda ya Ziwa kucheza mechi za Ligi Kuu Bara na wachezaji hao kubaki jijini Dar.

Tangu litokee sakata hilo kumekuwa na maneno mengi yakisemwa kwamba wachezaji hao wamesimamishwa na watakatwa sehemu ya mishahara yao, lakini Mazingisa amesema hamna kitu kama hicho.

“Hakuna mchezaji aliyeadhibiwa bali walisimamishwa kutokana na madai ya utovu wa nidhamu.

“Nilikutana na wachezaji hao na kuzungumza nao mambo yakaisha.

“Niseme tu, hili si kwa wachezaji pekee kwamba ndiyo wanapaswa kuwa na nidhamu bali kwa wote ili kuisaidia Simba kwenda inavyotakiwa ili mambo yaende kwenye mstari,” alisema Mazingisa.

4 COMMENTS:

  1. Hilo ndio jibu lililotegemewa na wengi. Key players majibu yake ndio huwa hayo..ila wangekuwa si key players majibu yangekuwa mengine. Asante Senzo kwa kuingia kwenye mfumo...ni kama Ajax na Chelsea... Cheza wewe sisi tukufunge

    ReplyDelete
  2. Wachezaji walisimamishwa nä viongozi wakaongea nao .Mlitaka nini zaidi .Tunawajua ni vyura. Nyondani ameingia mara nyingi kwenye matatizo ya ukosefu wa nidhamu.Amechuliwa hatua gani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Achana nao hao unajibishana na mkeo wa kazi gani wao wasubiri tu hiyo jumapili helua helua

      Delete
  3. uk replica omega shop online, combining elegant style and cutting-edge technology, a variety of styles of uk replica omega constellation shop online, the pointer walks between your exclusive taste style.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic