October 24, 2019


Bosi mkuu wa benchi la ufundi la Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amefunguka kuwa kichwa kinamchemka kutokana na dakika 270 ambazo ziko mbele yake kwenye Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo amesema hayo kutokana na ratiba ya Simba ambapo kabla ya jana Jumatano walikuwa na mechi dhidi ya Azam FC, kisha Jumapili watacheza na Singida United mkoani Arusha kisha watasafiri kuelekea Shinyanga kucheza na Mwadui FC.

Aussems amesema kuwa hiyo ni ratiba ngumu kwao kutokana na kucheza kwa karibu karibu lakini anaendelea kujiandaa kuona wanashinda kwenye mechi zote.

“Tuna mechi tatu zijazo za ligi ambapo tutaanza kucheza na Azam FC Jumatano, ambapo huu ni mchezo muhimu kwetu.

“Lakini pia tutakuwa na mechi dhidi ya Singida United na Mwadui FC. Mechi zote hizi zipo karibu zikiwa zinapishana kwa siku chache kila tutakapomaliza mechi moja, lakini hakuna namna zaidi ya kucheza.

“Kitu cha kwanza ni kuanza na mechi yetu ya kwanza kabisa dhidi ya Azam ambayo ndiyo ninaendelea kuifikiria namna gani nipate ushindi lakini pia kwenye mechi nyingine ambazo zitakuwa zimebaki nataka kuona tukishinda kwa ajili ya kujiongezea pointi tukiwa kileleni,” alisema Aussems.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic