WAARABU WA YANGA WAHAMISHIA VIKAO VYAO KIRUMBA
Ama kweli Yanga imepania kuwafunga wapinzani wao Pyramids ya Misri katika uwanja wa nyumbani kufuatia vikao vya mara kwa mara wanavyoweka kuelekea mchezo huo, huku jopo la viongozi likitua jijini Mwanza kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wachezaji.
Yanga inatarajia kushuka dimbani Oktoba 27 kuvaana na Pyramids katika mchezo wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Makamo Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick
Mwakalebela amefunguka kuwa, uongozi umejipanga kuhakikisha unapata matokeo mazuri, hivyo umeamua kuwa na vikao kwa ajili ya wachezaji na viongozi wa klabu hiyo ili kuwekana sawa.
“Kikosi chetu kipo vizuri tunashukuru, tumekuwa na mikutano ya hapa na pale na viongozi mbalimbali wa Yanga na wadau waliopo hapa lengo likiwa ni kukiandaa vyema kikosi chetu ili kiweze kufanya vyema katika mchezo wetu na Pyramids.
“Tutaendelea na vikao vyetu hadi siku ya mwisho ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wachezaji kuhakikisha wanafanikiwa kufanya vyema katika mchezo huo,” alisema Mwakalebela.
Aidha kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa, Rogers Gumbo, amesema wametua jijini Mwanza kwa ajili ya suala zima la uhamasishaji
Sasa hiyo habari ni ya Yanga au ya Pyramid? "Waarabu wa Yanga wahamishia vikao Kirumb" kichwa cha habari, ndani unazungumzia Yanga. Ongezeni weledi jamani
ReplyDeleteakili hamna hapo
Delete