October 19, 2019



MBWANA Samatta, nahodha wa timu ya Taifa ambaye ni Bwana Harusi mpya mjini ameipongeza timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa kupindua meza kibabe mbele ya Sudan kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya Kufuzu Michuano ya Klabu Bingwa Afrika itakayofanyika mwaka 2020 nchini Cameroon.

Stars ilishinda mabao 2-1 ikiwa ugenini ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 uwanja wa Taifa na kufanya isonge mbele kwa ushindi wa mabao 2-2 wakitumia faida ya bao la ugenini jambo lililoamsha hisia za watanzania wengi.

“Heshima kubwa mmetupa watanzania nasimama kwa heshima navua kofia yangu na ninawapigia saluti ya heshima asante sana na hongereni kwa kufuzu michuano ya Chan 2020 kama ilivyo ada basi hapohapo Sudan anzeni kunywa izo koka bili juu yangu,”

Mabao ya Stars yalipachikwa kimiani na Erasto Nyoni dakika ya 49 kwa mpira uliokufa na Ditram Nchimbi dakika ya 78 akimalizia pasi ya Idd Chilunda.

1 COMMENTS:

  1. Ila Amunike kaja kuchota pesa zetu akasepa zake huku watu wakimlilia azidi kuchota kusipolingana na uwezo wa kazi yaje.Tena waliokuwa wanamlilia ni watu wanaojifanya wa mpira? Hii nchi tulishazoea kupigwa rasili mali zetu huku tukiwaona wa maana wanaotupiga. Na akitokea raia mwema kukemea anaonekana mchawi. Watanzania tukiamka zaidi na kujitambua basi tutaonesha maajabu karibu kila idara uwezo tunao ila tunakosa kujitambua.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic