October 14, 2019


Inaelezwa uongozi wa klabu ya Pyramids FC ya Misri umetuma malalamiko kwenda Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ukigomea kitendo cha Yanga kubadilisha uwanja wa kuchezea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga itamenyana na Pyramids Oktoba 27 kwenye mechi ya raundi ya kwanza ambayo awali ilifahamika itanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam lakini baadaye Yanga wakaamua ichezewe Mwanza kwenye dimba la CCM Kirumba.

Kufuatia mabadiliko ya uwanja huo, imekuwa kama Pyramids wameshtukia na wameamua na taarifa zinasema wametuma malalamiko hayo CAF ili kujua sababu rasmi.

Taarifa zinasema Pyramids wanaona kama ni mbinu za Yanga kuwapoteza kwenye mechi hiyo mpaka imefikia hatua ya kuhoji CAF.

Timu hizo mbili zitakutana katika mechi hiyo ya Play Off ambapo mshindi atafuzu mpaka hatua ya makundi ya mashindano hayo.

5 COMMENTS:

  1. Hebu tufocus namna ya kuisadia Klabu ya Yanga ili ijiandae vizuri kwenye mapambano na sio kudeal ni kwanini wamehamisha mechi kuipeleka CCM Kirumba huu mjadala ufungwe tunapoteza muda kujadili mambo ya uwanja na tunaacha mambo ya msingi ambayo ni maandalizi kwa ajili ya mechi yenyewe!

    ReplyDelete
  2. Waandishi wa hiki chombo cha habari mmepitiliza mapenzi yenu kwa Simba kuliko kuandika habari kufuatana na miiko na kanuni za taaluma yenu

    ReplyDelete
  3. Nyie mbona mnateseka kwani mwandishi kajadili au katoa taarifa kwamba wamisiri wanalalamika tubadilikeni jamani hatuendelei kwasababu mnapenda kubeza taaluma zawatu ajiriwa wwe basi utoe taarifa afu simb inakujaje apo

    ReplyDelete
  4. Kweli watu wawache waandishi wafanye kazi zao wao wametoa taarifa kwa umma juu ya taaluma yao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic