KIONGOZI YANGA AUWASHA MOTO, AHOJI MBADALA WA GADIEL, AMTETEA ZAHERA
Aliyewahi kuwa kiongozi wa Yanga, Abdul Sauko, ameulaumu uongozi wa klabu hiyo kupitia Kamati ya Usajili kuhusiana na wachezaji waliosajiliwa, imeelezwa.
Kauli hiyo imekuja kufuatia timu yao kuwa na mwendelezo ambao si mzuri kwa msimu huu katika ligi na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taarifa imesema kuwa Sauko ameeleza wakati Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera anapendekeza majina ya wachezaji wanaopaswa kusajiliwa walipaswa kuwafuatilia.
Amefunguka kuwa si sahihi kumlaumu Zahera akisema walipaswa kushirikiana naye katika kuwafuatilia ili kijiridhisha juu ya uwezo wao na si kumlaumu.
Kiongozi huyo wa zamani ameilalamikia zaidi idara ya usajili huku akijaribu kutolea mfano baadhi ya wachezaji walioondoka kama Haji Mwinyi, Gadiel Michael na Heritier Makambo kuwa hakuna waliojaza nafasi zao.
0 COMMENTS:
Post a Comment