October 31, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza majina ya wachezaji ambao wataondoka leo kuelekea Misri kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC.

Kikosi kinachoondoka ni makipa, Farouk Shikalo, Metacha Mnata na Ramadhan Kabwili, mabeki ni Juma Abdul, Ally Ally, Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro na Mharami Said Issa ‘Marcelo’

Viungo ni nahodha Papy Tshishimbi, Feisal Salum ‘Fei Toto’ Mapinduzi Balama, Abdulazizi Makame, Deus Kaseke, Jaffar Mohammed huku mawinga ni Mrisho Ngassa, Patrick Sibomana na Issa Bigirimana, wakati washambuliaji ni Sadney Urikhob na Juma Balinya.


Katika mechi ya kwanza ikumbukwe Yanga ilipoteza kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCm Kirumba jijini Mwanza.

3 COMMENTS:

  1. MPIRA UNADUNDA BRO !! KATIKA DUNIA LOLOTE LINAWEZA TOKEA KWA KUDRA ZAKE MUUMBA.
    KILA LA KHERI YOUNG AFRICANS

    ReplyDelete
  2. Hivi Said Juma Makapu kwanini haondoki Yanga? Kwanini anaipenda timu isiyompenda? Sio hana kiwango bali kocha hamtski.Amwangalie Pato Ngonyani au Yisufu Mhilu walidharaulika Yanga huko waliko wanauwasha moto. Mhilu ana goli 4 angekuwa Yanga hadi leo asingecheza hata mechi moja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic