October 26, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera amesema kikosi chake kipo tayari kwa mapambano na amefanyia kazi matatizo kadhaa yaliyomo ikiwemo umaliziaji.

Zahera amesema ameandaa kikosi cha kufanya vizuri dhidi ya Pyramids lakini ana uhakika wa kutumia vizuri mchezo huo wa nyumbani.

Halikadhalika Kcha wa Pyramids, Sebastien Desabre raia wa Ufaransa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo dhidi ya Yanga SC Jumapili hii.

Desabre amesema wapinzani wao ni timu bora hivyo anaamini utakuwa mchezo mzuri na wenye upinzani kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Desabre ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari asubuhi hii jijini Mwanza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic