ZFF NA TFF LAIBUKA JINGINE JIPYA, MAMBO SASA NI ....
Baada ya jana kuibuka kwa taarifa ya Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF) kuvunja rasmi Mahusiano yote na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo ZFF kupitia kwa msemaji Adam Natepe wamesema kwasasa mahusiano yao kati ya mashirikisho hayo yanaenda vizuri kuanzia leo.
Kiongozi huyo amesema wamepanga kukutana kwa ajili ya kutatua changamoto zilizojitokeza kwa lengo la kujenga soka la Tanzania.
Natepe amesema leo Rais wa ZFF Seif Kombo Pandu amepigiwa simu na Rais na Katibu wa TFF kwaajili ya kupanga na kurejesha uhusiano mzuri kati yao.
Zoog kubwa lililokuwepo ni kuhusiana na suala la mgao wa fedha za FIFA ambazo ZFF walikuwa wanadai hawapatiwi na TFF.








0 COMMENTS:
Post a Comment