October 27, 2019




FT: Yanga 1-2 Pyramids

Dakika ya 90+4 Juma Abdul alipiga faulo iliyomkuta All akapaisha
Dakika ya 90+2 yondani anaonyeshwa kadi ya njano ya pili na kupewa nyekundu
Dakika za nyongeza 5

Dakika 90 zimekamilika
Dakika ya 87 Tshishimbi anaandika bao la kwanza akimalizia pasi ya Deus Kaseke

Dakika ya 86 Patrick Sibomana anaingia akichukua nafasi ya Makame
Dakika ya 87 wanaanza kona fupi, Shikalo anaokoa
Dakika ya 86 mpira unasimama kwa muda 
Dakika ya 82 Johe Atwi anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Ally

Dakika ya 77  Yondani njano dakika ya 77
Ngassa dk ya 71 anaingia Kaseke
Fei Toto dk ya 68 Juma Balinya
Makame njano dakika ya 62
Dakika ya 62 Goal la pili Mohamed Fathy
Dakika ya 62 Ngassa anapiga konaDakika ya 61 Tshishimbi anapiga pasi ndefu ambayo haimkuti mchezaji, waarabu wanaanzisha taratibu, Sadney anajaribu shambulizi linatoka nje
Dakika ya 60 Sonso anaokoa hatari huku waarabu wakipungua kasi ya kushambulia kwa sasa
Dakika ya 59 All anaokoa hatari na kuanzisha mashambulizi

Dakika ya 58 Ahmed anapiga shuti nje ya 18 Shikalo analiokoaDakika ya 57 Fei Toto anapiga bonge moja ya bao linapanguliwa na mlinda mlango Ahmed Elshanawy na kuzaa tunda iliyopoteaDakika ya 54 Abubakari anarusha mpira vibaya, Sadney anachezewa rafu
Dakika ya 52 kadi ya njano kwa Ahmed Mansour wa Pyramids


Dakika ya 50 Yondani anaokoa mpira ndani ya 18
Kipindi cha pili kimeanza

Mapumziko
Yanga 0-1 Pyramids Zimeongezwa dakika mbili
Dakika 45 Fei Toto kwake Ally, Sidney, Tshishimbi Mapinduzi anapambana mpira unatoka nje Dakika ya 44 Shikalo anaanza na Ally Ally 
Dakika ya 43 Yanga wananzisha mashambulizi
Dakika ya 42 Waarabu wanafunga goal kupitia kwa Erick Traory akiwa nje ya 18
Dakika ya 41 waarabu wanaanzisha mashambuliziDakika ya 40 Ngassa anatoa mpira nje
Dakika ya 39 Shikalo anaanzisha mashambulizi kwa Yanga, All anaokoa ndani ya 18
Dakika ya 38 Waarabu wanacheza faulo kwa All All Dakika ya 37 Makame anaokoa shambulizi ndani ya 18Dakika ya 35 Shikalo anaanisha mashambulizi kwenda kwa waarabu
Dakika ya 34 Juma Abdul anatafuta njia kwenda kwa waarabu
Dakika ya 33 Pyramids wanaanzisha mashambuliziDakika ya 32 Waarabu wanafanya shambulizi kwa Yanga
Dakika ya31 Shikalo anaanzisha mashambulizi kwenda kwa waarabu

Dakika ya 30 Sonso kwa Ally Ally wanapoteza umiliki Yanga.

 Dakika ya 29 Papy Tshishimbi anaonyeshwa kadi ya njano

Dakika ya 28 Waarabu wanapaisha kwa Shikalo
Dakika ya 27 Mrisho Ngassa anaonyeshwa kadi ya njano kwa kucheza rafu
Dakika ya 26 Sidney anacheza rafu akiwa ndani ya 18
Dakika ya 25 Yanga wanarusha kwenda kwa waarabu
Dakika ya 24 Ally Ally anapeleka mashambulizi kwa Waarabu

Dakika ya 23 Sonso anapiga mpira wa adhabu hauzai matunda 
Dakika ya 22 Juma Abdul anapiga faulo inapigwa kichwa na Ally Ally inapaa anaganiDakika ya 21 Ngassa anapiga faulo haileti matunda
Dakika ya 20 Juma Abdul anachezewa rafu na waarabu

Dakika ya 19 Free kikck ya waarabu haizai matunda

Dakika ya 18 nahodha wa Pyramids anachezewa rafu na Ally Dakika ya 17 Mlinda mlango wa Mwarabu anataka kufanyiwa huduma ya kwanza
Dakika ya 16 Fei anacheza faulo kwa mwarabu
Dakika ya 15 Fei Toto anampa Makame safari kwa waarabu
Dakika ya 14 mchezaji wa mawarabu anacheza faulo kwa kugusa mpira.
Dakika ya 13 Yondani anaanzisha mashambulizi kwenda kwa waarabu
Dakika ya 12 Waarabu wanaanzisha mashambulizi
Dakika ya 11 Shikalo anaokoa shuti lililopigwa nawaarabu ndani ya 18.

Dakika ya 10 Kelvin Yondan amekoa hatari iliyokuwa inazama ndani ya nyavu jumla

MCHEZO wa kimataifa kati ya Yanga na Pyramids unaendelea uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mashabiki wamejitokeza kuipa sapoti Yanga ambao ni wawakilishi pekee wa kimataifa kwa Tanzania.

Mpaka sasa hakuna timu iliyoona lango la mpinzani ikiwa ni kipindi cha kwanza.

10 COMMENTS:

  1. usijali watapindua meza mbele ya mapiramidi

    ReplyDelete
  2. Watapinduwa meza mechi ya marudiano.Yanga Oyeeeee

    ReplyDelete
  3. Mji kimyaaa .Aibu ya kufungwa nyumbani .Msiende Misri au pelekeni na gunia la magoli.Bila Yondani itakuwa mauaji ya halaiki.

    ReplyDelete
  4. kwanza nitoe pole kwa klabu yangu kufungwa dhidi ya piramid leo tena nyumbani,
    lakini huu ni ujumbe kwa locha zahera aache umungu na maneno mingi katika kazi. mpira hauhitaji maneno mengi ni kazi tu.
    Nani hajui uwezo wa nafasi ya Sadney, ni mchezaji anayeweza sana kuanzisha mashambulizi na si mfungaji. lkn leo ndio alipewa jukumu la kuwa mfungaji, waarabu walipoona kuwa yanga hawana mfungaji ikabidi waache beki wawili ili washambulie na kukimaliza kiumgo cha yanga na kupoteza mawasiliano
    Pamoja na madhaifu ya yanga lkn ni wazi refa wa leo wote walikuja na mipango yote, mechi ilikuwa kavu ile lkn refa anapuliza faulo za kijinga na waarabu walitumia sana ujanja kwa maelekezo ya refa.ona refa alivyoamua kuimaliza mechi kwa kumlima umeme yondani ili kuhakikisha yanga hatoboi kimataifa.
    TFF muliangalie hili, nawe zahera, hebu ona alivyoingia sibomana na mwenzake kazi ilivyoonekana sio lazima kila siku kumtumia fei toto, lazima ukubali kuwa umeshindwa kumrudisha toto katika kiwango kile,
    kwangu mm leo aliyefungwa si yanga bali ni kocha
    yanga mrudi kujipanga katika ligi na si kutegemea kimataifa huko mmeshatolewa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga ilianza kukosea tangu kwenda mkoani na kuacha sapoti ya mashabiki wengi Dar hivyo katika uwanja wote walikuwa wageni. Lakini pia kuhusu kadi ya Yondani wa kulaumiwa ni Ally Sonso na si refa, mwingine ni Ngasa kwa kusababisha goli la pili kwani alikuwa na uwezo wa kuufany chochote ule mpira lakini akatumia ukongwe wake vibaya. Kuna mwandishi aliandka hapa hapa kwamba baada ya kubadili uwanja tubadili na mbinu lakini wapi! Mimi nilijua Zahera alivumiliwa yanga kwa sababu Yanga ilikuwa katika hali ngumu kiuchumi lakini bado yupo. Tutaendelea kulalamika wakati tatizo linaonekana. Mwanzo alikuwa anajitetea kuwa wachezaji hawana muunganiko mzuri sasa hadi leo hawajazoeana tu? Basi tusubiri mapinduzi ya meza.

      Delete
  5. Swali Shishimbi si alipewa kadi mbili za njano

    ReplyDelete
  6. Kevin Yondani alipewa kadi halali baada ya kufanya professional Gould baada ya Ali Sonso kupoteza mpira.Asingefanya hivyo lilikuwa goli la tatu. ALI TAKE ONE FOR THE TEAM.

    ReplyDelete
  7. Yondani ameishazeeka na amekomaa!anatakiwa kuacha ujinga kama kutemea mate wachezaji wenzake. Mechi na polisi alimpiga teke mchezaji mwenzake sehemu za siri na mpira haukuwa karibu na pale. Juzi dhidi ya Mbao akijua nyuma yake kuna mchezaji akarukia mpira kakunja na teke la nyuma kamkanyaga mtu tumboni...matukio yote mawili alistahili red card.Alidhani ataendelea na ujinga huo katika mchezo wa kimataifa..,haya kazuia goli la tatu (mpaka sasa Pyramid wana goli la ugenini hivyo ni 3-1).Je kukosekana kwake misiri hakutazuia magoli..Aache utoto keshakuwa.,rafu zisizo na tija za kishenzi ni ujinga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic