MAGORI APEWA MAJUKUMU MAPYA SIMBA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji amemteua aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu, Crescentius Magori kuwa Mshauri Binafsi wa Mwenyekiti wa Bodi.
Magori ambaye amewahi kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Mjumbe Kamati ya CAF ya Soka la Ufukweni na Futsal, Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Baraza la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Mwenyekiti wa Fedha na Mipango wa TFF na Mjumbe wa Kamati za Masoko wa TFF atakuwa na jukumu la kumshauri mwenyekiti mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuboresha utendaji ambao utawezesha klabu kupata mafanikio zaidi.
Uteuzi wake umeanza jana Jumatano Oktoba 23, 2019.
Kwa niaba ya Wanasimba, tunamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya tukiamini kwamba atatoa msaada mzuri kwa klabu ambao utatuwezesha kupiga hatua kubwa na hasa kutokana na uzoefu wake mkubwa kwenye soka.
0 COMMENTS:
Post a Comment