RAHEEM Sterling leo ameonyesha maajabu yake baada ya kufungua akaunti ya mabao kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Aston Villa wakiwa uwanja wa nyumbani wa Etihad.
Dakika ya 46 alianza kucheka na nyavu kabla ya dakika 13 mbele Kevin de Bruyne kupachika bao la pili dakika ya 65 na lile la tatu kupachikwa dakika ya 70 na Iikay Gundogan.
Ushindi wa leo wa mabao 3-0 uliingia doa dakika ya 87 baada ya Fernandinho kuonyeshwa kadi nyekundu.
Ushindi huo unairudisha City kwenye ushindaniikiwa nafasi ya pili dhidi ya Liverpool wakiwa na pointi 22 baada ya kucheza michezo 10 tofauti ya mchezo mmoja na Liverpool yenye pointi 25 imecheza mechi 9 ikiwa nafasi ya kwanza.








0 COMMENTS:
Post a Comment