October 26, 2019


LICHA ya nahodha wa timu ya Genk, Mtanzania Mbwana Samatta kuvaa kitambaa cha unahodha kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya bado mambo yamekuwa magumu kwa timu yake.

Kupoteza kwa kufungwa mabao 4-1 mbele ya Liverpool kumeifanya timu yake kubaki mkiani ikiwa na pointi moja kibindoni.

Samatta alifunga bao dakika ya 27 kwa kichwa mbele ya James Milner na mpira ulinjaa wavuni ila VAR ililikataa hilo bao kwa kudai kuwa aliyepiga pasi ya bao aliotea.


Kwenye kundi E Napol inaongoza ikiwa na pointi 7 ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi sita na Salzburg ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu baada ya kucheza mechi tatu.

Samatta amefunga bao moja mpaka sasa kwenye mechi tatu walizocheza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic