October 19, 2019


Licha ya habari kuzagaa kuwa amewahi kutoka kimapenzi na staa wa muziki wa Injili, Rose Muhando, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, ameibuka na kujibu tuhuma hizo kwamba katika maisha yake ya usambazaji wa kazi za wasanii hajawahi kujihusisha nao kimapenzi hata mmoja.

Msama aliiambia Shusha Pumzi kuwa hajawahi kutoka na Rose na hatarajii kutoka na mwimbaji yeyote kwa sababu yeye ni mtumishi wa Mungu hivyo endapo kuna mtu ana ushahidi wowote wa kubanjuka naye, basi autoe maana ana kovu sehemu hivyo huyo atakayejitokeza aseme liko wapi kwenye mwili wake.

“Tangu nianze kufanya kazi ya usambazaji wa kazi za muziki wa Injili sijawahi kutoka na mwimbaji yeyote na sitarajii maana nampenda Mungu, kama kuna mwanamke kwenye tasnia hiyo anayesema amewahi kutoka na mimi kimapenzi, basi na ajitokeze kiroho safi kabisa maana watu wamekuwa wakizungumza sana,” alisema Msama.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic