October 23, 2019


Kikosi cha Simba leo kitashuka uwanjani kuwavaa wapinzani wao Azam FC bila ya nyota wake watatu muhimu katika mchezo huo. Timu hizo zinatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbelgiji, Patrick Aussems alisema wachezaji hao watakosekana kutokana na tatizo la majeraha.

Aussems aliwataja wachezaji hao ni kiungo Jonas Mkude, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ waliopata majeraha wakiwa kwenye timu ya taifa, Taifa Stars iliyofuzu kucheza Chan hivi karibuni walipocheza na Sudan.

Alimtaja mchezaji mwingine ni beki Shomari Kapombe ambaye yeye alijitonesha enka yake, hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi hicho kitakachoivaa Azam.

“Katika mchezo wetu wa kesho (leo) dhidi ya Azam ninatarajia kuwakosa wachezaji wangu watatu muhimu ambao ni Mkude, Tshabalala na Kapombe kutokana na
majeraha.

“Hivyo hawatakuwa sehemu ya kikosi changu, lakini nikiwakosa wachezaji hao tayari ninao wengine watakaocheza katika nafasi zao vizuri. “Kwa upande wa Mkude nafasi yake atacheza Fraga (Gerson), Kapombe ni Shamte (Haruna) na kwa Tshabalala yupo Gadier (Michael),”alisema Aussems.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic