October 31, 2019


Na Saleh Ally

Nimeona katika Makundi kadhaa ya Whatsapp kuwa kipa Aishi Manula amechoka na anapaswa kupumzishwa, wanaona hata kupoteza Kwa Simba kwa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC ni sababu yake, hawajiulizi maswali mengine kwa nini washambulizi au viungo hawakufunga.

Kuna kipindi mashabiki wanaweza kujifunza KUWAHESHIMU wachezaji wao hata baada ya timu wanazozishabikia kupoteza mchezo.

Soka, hakuna timu iliyoshinda kila mchezo na hii ndio raha ya mchezo huu.

Mashabiki wengi hapa nyumbani wanaamini kulaumu ndio kushangilia au kushabikia. Wakati mwingine vizuri kuangalia mpira na kuburudika lakini vizuri kujifunza kinachotokea.

HISIA au kusikia na kuunga tu mkono hata bila kujaribu kutafakari kumesababisha KUADHIBIWA kwa wachezaji wengi sana, jambo ambalo hawakustahili.

Kumbukeni, kama ulivyo wewe unayeshabikia, Wachezaji nao ni binadamu. Kuna siku wanaamka vibaya na kushindwa kufanya kile unachokitarajia... Pia Kumbuka, mchezo wa soka unaendwa sana kwa kuwa HAUJAWAHI kutoa furaha ya milele KWA UPANDE MMOJA TU.

3 COMMENTS:

  1. goli kama alilofungwa manula ni goli gumu kwa kipa yoyote yule

    ReplyDelete
  2. Naona imekuuma Sana Kwa kusemwa manura mbona haijakuuma mwinyi zahera walivyomfanyia vurugu mwanza Leo wanaona hawafai wakati msimu uliopita walimuona ndio shujaa mbona haujalipinga ilo ??,hacha unazi wewe manura kachoka sana

    ReplyDelete
  3. Kiukweli umefika wakati ambao Beno Kakolanya inabidi apewe nafasi ili naye aonyeshe uwezo maana kwa sasahivi uwezo wa Manula unafahamika vya kutosha, hakuna jipya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic