October 31, 2019


Wakati kikosi cha Yanga kikitarajia kukwea pipa leo kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids, baadhi ya wachezaji watabaki.

Wachezaji hao watabaki kutokana na sababu mbalimbali ambazo hazitawaruhusu kusafiri na wenzao kwa ajili ya kibarua hicho kizito.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amewataja wachezaji hao ambapo mmoja wao ni David Molinga 'Falcao'.

Aliwataja nyota hao wanaobaki ni Selemani Mustafa na Molinga ambao vibali vyao haviruhusu kucheza hatua hii, huku Kelvin Yondani akitumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyopata katika mchezo uliopita.

“Timu inaondoka na wacheza 20, baada ya kutoka Mwanza, imeendelea na mazoezi leo (jana), uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini chini ya kocha wetu Mwinyi Zahera,” alisema Bumbul

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic