BEKI mkongwe wa kati wa Simba Muivory Coast, Pascal Serge Wawa ametamba kuwa usajili uliofanywa na watani wao Yanga haumpi hofu ya Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwenda Jangwani.
Kauli hiyo aliitoa ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo wao mgumu wa Ligi Kuu Bara waliocheza na Azam FC jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga iliyowasajili wachezaji baadhi kama David Molinga, Lamine Moro na Patrick Sibomana hivi sasa inapambania ubingwa huende kwao kwenye msimu huu baada ya kuukosa kwa misimu miwili mfululizo uliokwenda Simba kwa vipindi vyote.
Akizungumza na Spoti Xtra, Wawa alisema kuwa malengo yake ni kucheza mafanikio akiwa na Simba kwa vipindi vyote atakapokuwepo hapo kwa kuhakikisha anachukua mataji ya ligi.
Wawa alisema kuwa hana hofu ju ya hilo kutokana na ubora wa kikosi chao, maandalizi mazuri ya ‘pre season’ waliyoyafanya wakiwa chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbelgiji, Patrick Aussems.
“Katika maisha yangu ya soka, sijawahi kufi kirii kufungwa, kutoa sare zaidi ya ushindi pekee na hiyo ni kutokana na malengo yangu niliyojiwekea.
“Hivyo, ninaamini ninapopata matokeo mazuri ya ushindi yananijengea mazingira mazuri ya ubingwa na ndiyo sababu nikiwa uwanjani ninatimiza majukumu yangu ya kuokoa na kupunguza hatari golini kwangu.
“Ninafahamu kila timu ina malengo ya kuchukua ubingwa wa ligi msimu huu ziiwemo timu kubwa za Simba na Yanga, lakini niwaambie kuwa wasahau hilo,”alisema Wawa.
Huo ndio ukweli watasubiri sana.Back to back 10 years.Simba oyeeee
ReplyDelete