DITRAM Nchimbi nyota anayekipiga timu ya Polisi Tanzania inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za kutua kwenye klabu ya Yanga wakati wa usajili wa dirisha dogo.
Yanga kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kusuka kikosi kipya kitakacholeta ushindani kwenye ligi baada ya kutolewa kimataifa na timu ya Pyramids jana kwa jumla ya mabao 5-1.
Habari zinaeleza kuwa kwa sasa tayari mazungumzo yameanza kufanyika ili kumpata nyota huyo asaidiane na David Molinga ambaye ameonekana kuingia kwenye mfumo wa Zahera.
Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Geofrey amesema kuwa hakuna tatizo kwa Yanga kuipata saini ya nyota huyo iwapo taratibu zitafuatwa.
"Kama wao wanamtaka Nchimbi hakuna shida maisha ya mchezaji ni kucheza sasa utaratibu upo wazi jukumu lao itakuwa ni kukaa mezani pia wanapaswa waongee na Azam FC ambao wao ndio mchezaji wao," amesema.
Nchimbi ametupia jumla ya mabao matatu ndani ya Ligi Kuu Bara pia ni nyota aliyefanya vizuri kwenye michuano ya Chan nchini Sudan kwa kufunga bao la ushindi akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania.








Dawa ya Mgonjwa ni kufanya upasuaji ili kuondoa kiini cha ugonjwa sio kumpatia chakula ukitegemea kiini kitaondoka....Tatizo ni benchi la ufundi limefikia ukomo wa uwezo hiki ndicho chanzo cha mashabiki kushinikiza kuondolewa kwa Kocha au Mabadiliko kufanyika. Hata ukisajili akina Messi na Ronaldo kama ufundishwaji ni poor usitegemee ushindi. Yanga hii inahitaji uwekezaji bora ambao unaendana sambamba na benchi la ufundi lililo bora....Uongozi wa Yanga unajivutavuta na kujificha kwenye kichaka na kivuli cha Zahera lakini ukweli ni kuwa Kocha huyu hatawafikisha popote....mbinu zimegota...
ReplyDelete