PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kiwango cha wachezaji wake jana mbele ya Mbeya City kilikuwa bora licha ya kukosa nafasi nyingi za mabao.
Simba jana ilishinda mbele ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Uhuru kwa jumla ya mabao 4-0 ushindi uliowafanya wazidi kujikita kileleni wakiwa na pointi 21.
"Wachezaji walijituma na walifanya kazi kwa umakini licha ya kukosa nafasi nyingi za wazi, kwa namna tulivyokuwa tukicheza tulikuwa na nafasi ya kushinda mabao mengi zaidi ya yale tuliyopata," amesema.
Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere, Clatous Chama, Shiboub na Deo Kanda.







0 COMMENTS:
Post a Comment