RAMADHAN
Nswazurimo, Kocha Mkuu wa Singida United amesema kuwa kinachoiponza timu yake
kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zake ni kushindwa kujiamini kwa
washambuliaji wake.
Singida
United ikiwa imecheza juma ya mechi 10 sawa na dakika 900 imefunga jumla ya
mabao mawili pekee huku ikiruhusu kufungwa jumla ya mabao 10 ikijikusanyia
pointi nne pekee.
Nswazurimo
amesema kuwa wachezaji wake wanashindwa kujiamini wakiwa na mpira jambo
linalowafanya washindwe kufunga licha ya kuwa na nafasi nyingi ndani ya uwanja.
“Nimegundua
kwa sasa tatizo kubwa kwa washambuliaji wangu ni kushindwa kujiamini wakiwa na
mpira ndani ya eneo la hatari hata wakiwa nje ya 18 wanashindwa kufanya
maamuzi.
“Tayari
nimegundua namna bora itakayowarejesha kwenye ubora na kwa kuanza nitaanza
kuwajenga saikolojia yao ili wawe makini katika umalizaji wa nafasi ninaamini
tutafanya vizuri,” amesema Nswanzurimo.







0 COMMENTS:
Post a Comment