OBREY Chirwa
kiongozi wa safu ya ushambuliaji wa Azam yenye wakali wawili Donald Ngoma na
Idd Seleman ‘Naldo’ leo wamepewa kazi ngumu ya kuipa pointi tatu mbele ya
Kagera Sugar.
Azam FC ipo
chini ya Kocha mpya, Arstica Cioaba alipoteza mchezo wake wa kwanza mbele ya
Ruvu Shooting kwa kufungwa bao 1-0 leo atarusha kete yake ya pili mbele ya
Kagera Sugar uwanja wa Azam Complex.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Azam FC Idd Cheche amesema kuwa
wamegawa majukumu kwa washambuliaji wao wakiongozwa na Chirwa ili kupata
matokeo chanya.
“Kwenye ligi
kikubwa kinachotafutwa ni matokeo jambo hilo limetufanya tufanye kazi na safu
ya ushambuliaji kwa kuwapa maelekezo mapya na majukumu mazito kushirikiana na
wengine ili kupata ushindi.
“Kikubwa
tumewaambia wawe watulivu wakiwa eneo la hatari na kufanya maamuzi kwa usahihi
hivyo Chirwa, Ngoma na Naldo wana kazi ya kuwaongoza wachezaji wenzao kutafuta
ushindi tunajua mchezo utakuwa mgumu,” amesema Cheche.







Ngoma droo hakuna mbabe leo.but the time will tell lets wait.
ReplyDelete