HITIMANA
Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kinachomkwamisha kupata matokeo kwa
sasa ugenini ni kuwa na majeruhi wengi ndani ya timu yake jambo linampasua
kichwa kwenye upangaji wa kikosi.
Namungo FC
ambayo imepanda ligi msimu huu imeshindwa kufurukuta kwenye mechi zake zote
tatu za ugenini kwa kuruhusu vichapo huku ikikaza ikiwa nyumbani kwa
kujikusanyia jumla ya pointi 13.
Namungo
imepoteza jumla ya pointi tisa ugenini ilianza mbele ya KMC kwa kukubali
kuchapwa bao 1-0 kisha ikafuata mbele ya Azam FC kwa kufungwa mabao 2-1 kabla
ya kupoteza mbele ya Kagera Sugar kwa kufungwa mabao 2-0.
Ikiwa uwanja
wa Majaliwa, Namungo haijapoteza mchezo hata mmoja kati ya mitano iliyocheza na
iliambulia sare moja ya bila kufungana mbele ya Mwadui FC na kushinda mechi
zote nne mbele ya Ndanda FC mabao 2-1, Mtibwa Sugar bao 1-0, Lipuli bao 1-0 na
Singida United kwa mabao 2-0.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa mechi nyingi za ugenini amekuwa
akichezesha wachezaji wake wengi wakiwa ni majeruhi jambo linalomnyima matokeo.
“Kwa sasa
kikosi changu hakipo sawa wachezaji wangu muhimu ni majeruhi na nimekuwa
nikiwachezesha baadhi kutokana na kukosa mbadala wake kwa mfano Lukas Kikoti mbele
ya Kagera Sugar nilimpanga pamoja na Bigirimana Blaise.
“Kwa sasa
tunaangalia namna wachezaji watakavyoamka kwani tuna mchezo dhidi ya Ruvu
Shooting na tutakuwa nyumbani tunaomba mashabiki watupe sapoti,” amesema.







Mbona nyumbani wanashinda? Au wakicheza nyumbani hao majeruhi wanapona ghafla na kupata matokeo?
ReplyDelete