November 7, 2019


Nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi, raia wa DR Congo, amewapiga biti wapinzani wao Simba kuwa kwa msimu huu watawapokonya ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa ajili ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo inasimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Tshishimbi ameweka wazi hilo baada ya Yanga kuondoshwa katika Kombe la Shirikisho Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 5-1 na Pyramids ya Misri katika hatua ya mtoano.

Kiungo huyo aliyetua Yanga misimu miwili nyuma akitokea Mbabane Swallows ya Eswatini, ameliambia Championi Jumatano, kuwa kwa sasa wanachotaka ni kushinda ubingwa wa ligi ambao unamilikiwa na Simba kwa ajili ya kujiweka katika nafasi nzuri ya kurejea katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu ujao.

“Hatuwezi kukata tamaa kwa sababu tumetoka katika michuano ya kimataifa, tutaendelea kupambana na tutajitolea kuchukua ubingwa kwa ajili ya kurudi tena katika mashindano ya kimataifa.

“Kitu kikubwa mashabiki wetu waendelee kutusapoti tu kwani kilichotokea ni mambo ya mpira. Kwa sasa tunataka pointi tatu katika mechi zetu za ligi na hatuwezi kusema kwa sababu tumefungwa kimataifa ndiyo tufungwe na huku.

“Tunajiandaa na mechi yetu ya ligi na lengo ni kutwaa pointi tatu tu katika kila mechi ambayo tutakuwa tunaicheza kwa sasa,” alimaliza Tshishimbi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic