November 7, 2019


MASTAA wa Yanga wamepoteza takriban Sh Mil. 200 walizoahidiwa na matajiri wa timu hiyo kama wangefanikiwa kuwaondoa wapinzani wao Pyramids FC ya nchini Misri.

Wachezaji hao waliahidiwa fedha hizo kama wangefanikiwa kuwaondoa wapinzani wao hao kwa kuwafunga ugenini na kuwatoa kwenye hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga katika mchezo huo walikuwa wanatakiwa kuwafunga Pyramids mabao 2-0, ili wawaondoe katika michuano hiyo lakini wakafungwa 3-0.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano kutoka kwa mmoja wa wachezaji wa Yanga, waliahidiwa fedha hizo vyumbani kabla ya kuingia vyumbani kujiandaa na mchezo huo.

“Kama mlikuwa mnafuatilia kwa ukaribu mchezo huo tuliocheza na Pyramids utaona kila mchezaji alipambana kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri.

“Na tulikuwa tunapambana kutokana na ahadi kubwa ya fedha tuliyowekewa na mabosi wetu wakiwemo wadhamini wetu GSM ambao walitoa Sh mil 30 tofauti na matajiri wengine.

“Na kwa haraka tulipiga hesabu ya haraka kwa kila mchezaji kuondoka na Sh Mil. 10 ambazo tumezikosa, tumesikitika sana,” alisema mtoa taarifa wetu ambaye ni mchezaji.

Alipoulizwa nahodha msaidizi wa timu hiyo, Juma Abdul kuzungumzia hilo, alisema kuwa: “Ni kweli hizo taarifa ulizozisikia, tumeumia kupoteza fedha hizo tulizoahidiwa lakini hakuna jinsi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic