KOCHA ARSENAL AKALIA KUTI KAVU
Unai Emery amepewa mwezi mmoja kuokoa kazi yake kama mkufunzi wa Arsenal. (Mirror)
Kiungo wa kati wa England Adam Lallana, 31, analengwa na vilabu vya China na ligi kuu ya soka, huku mkataba wake na Liverpool ukielekea kumalizika. (Telegraph)
Arsenal imejitenga na tetesi kuwa huenda ikamuajiri Jose Mourinho kama kocha wao mpya. (ESPN)
Mkuu wa soka wa Arsenal, Raul Sanllehi, ameripotiwa kuonekana akila chakula cha jioni na Mourinho lakini wawili hao hawajazungumza kwa miaka kadhaa.(London Evening Standard)
Arsenal imejitenga na tetesi kuwa huenda ikamuajiri Jose Mourinho
Kocha wa zamani wa Juventus Max Allegri, ambaye aliwahi kuhusishwa na Arsenal, anapigiwa upatu kujiunga na Bayern Munich baada ya Niko Kovac kuondoka. (Bild, via Football Italia)
Meneja wa Leipzig Ralf Rangnick pia amehusishwa na nafasi ya ukufunzi iliyoachwa wazi Bayern Munich - naye Jose Mourinho akiwa mmoja wa wale wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo. (London Evening Standard)
Salzburg bado haijapokea ofa kutoka usajili wa mshmbuliaji wa Leeds-mzaliwa wa Norway, Erling Braut Haaland, 19, ambaye amehusishwa na vilabu vya Manchester United, Real Madrid na Juventus. (Mirror)
Mshmbuliaji wa Leeds Erling Braut Haaland ananyatiwa na Manchester United, Real Madrid na Juventus
Roma inajiandaa kufanya mkutano na Manchester United kuhusu mkataba wa kudumu wa beki wa England Chris Smalling na iko tayari kulipa euro milioni 10 kumpata kiungo huyo wa miaka 29. (Calciomercato)
Kiungo wa kati wa Manchester City, Mhispania David Silva, 33, anatarajiwa kukosa mechi ya Jumapili ya ligi ya premia watakapuzuru Liverpool baada ya kuumia misuli. (Mirror)








This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteSalehe Jembe jaribu kuhakiki habari kabla ya kupost, Erling Haaland sio mshambuliaji wa Leeds ni mshambuliaji wa Salzburg ya Austria , Baba yake Braut Haaland ndio aliwahi kuchezea Leeds kabla ya kuhamia Manchester City . Erling alizaliwa Leeds England ila ni raia wa Norway. kila kukicha blog yako huwa inawadaganya wadau.
ReplyDelete