November 6, 2019


MBWANA Samatta nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ametimiza ndoto yake ya kuifunga timu kubwa duniani ambao ni mabingwa wa Ulaya, Liverpool.

Kwenye mchezo ambao unaendelea kwa sasa uwanja wa Anfield kati ya Liverpool na Genk,Samatta amefunga bao lake la pili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya huku leo bao lake la pili akiwatungua Liverpool dakika ya 41 kwa kichwa matata kilichotinga nyavuni.

Genk ipo nyuma kwa sasa kwa mabao 2-1 ambayo yamefungwa na wenyeji wao Liverpool, Jurgen Klopp Meneja wa Liverpool alipoona namna Samatta akipachika bao alicheka kwa furaha.

Ngoma imekamilika kwa Genk kupoteza mchezo wa leo kwa kufungwa mabao 2-1.

1 COMMENTS:

  1. Hahahaha Mara mechi inaendelea kwa sasa mara ngoma imekamilika duh

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic