November 6, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umemtanga aliyekuwa Ofisa Habari na sasa Ofisa Masoko, Dismas Ten kuwa Meneja wa timu.

Ten amepewa majukumu hayo kwa muda ili kushikilia kiti alichokuwa amekikalia Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye aliondolewa ndani ya nafasi hiyo.

Nafasi hiyo atakaa nayo Ten kwa muda maalum mpaka pale atakapopatikana mtu mwingine ambaye atachukua nafasi hiyo.

Mbali na Ten, mchezaji wa zamani ndani ya Yanga, Said Maulid 'SMG' amechukua kiti cha Noel Mwandila kama msaidizi wa Boniface Mkwasa ambaye ametangazwa kuwa Kaimu Kocha Mkuu kufuatia klabu kvunja mkataba na Mwinyi Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic