November 5, 2019


Ijumaa ya wiki iliyopita kiungo Jonas Mkude alichelewa mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yakifanyika Viwanja vya Gymkhana, Posta, Dar sasa jana tena mchezaji huyo amerudia ya wiki iliyopita. Mkude ambaye ni kati ya viungo wakabaji bora Bongo, ndiye mchezaji mkongwe Simba ambako ndipo alipoanzia soka lake.

Sasa twende mazoezini; wiki iliyopita uwanja uleule, tabia ileile ya kuchelewa aliionyesha ambapo alifika mazoezini wakati wenzake wameshafanya kwa zaidi ya dakika 15 tena akiwa ndani ya ndinga kali aina ya Toyota Harrier.

Alipofika tu, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemanu alionekana kuchukizwa na kitendo cha Mkude kisha akamuonya kwa kumtaka kutorudia tena.

Sasa juzi Ijumaa, kwa mara nyingine Mkude alifika mazoezini na kukuta wenzake wanaelekea kumaliza mazoezi, akapaki gari yake aina ya Toyota Harrier huku akiwa amevalia kaptura ya jinzi iliyochanwa kisasa kwenye mapaja na juu alivalia fulana nyeusi.

Wakati akiingia uwanjani hapo, meneja alionekana akimuagiza mpiga picha wa timu hiyo ampige Mkude kama ushahidi. Moja kwa moja alikwenda kuonana na Rweyemamu kisha kocha wa viungo, Adel Zrane, hawa wote walionekana kutofurahishwa na kitendo hicho.

Rweyemamu aliliambia Championi Jumamosi kuwa, Mkude atajadiliwa kwenye kikao cha viongozi wa Simba chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingiza ambaye ni raia wa Afrika Kusini. Ikumbukwe Mkude aliachwa katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Singida United na Mwadui FC kutokana na kutokuwa sawa kimwili.

3 COMMENTS:

  1. Katika maisha mtu anapovuta umri ndipo anapokuwa na hekima kutokana na aliyoyaona na ndipo anapojirekebisha na jkujijutia yale aliyoyafanya hapo nyuma na kuwausia vijana namana ya kuishi vema kufuatana na hali ya maisha ilivo na awe mfano Kwa kuwausia wengine lakini ni jambo la kusikitisha wengine huenda kinyume na hayo

    ReplyDelete
  2. Kashajiona yeye ndio bora kuliko simba ameshasahau ametolewa wapi huo umaarufu bila simba angeupata wapi? Hiyo ndio shukurani ya binadamu

    ReplyDelete
  3. Huyo jamaa ana body ya mpira angekuwa serious na mpira asingekuwa bongo,dah sa harrier ndo kitu gn,age inaenda hawajifunz kutoka kwa boban aliridhika na soka ya bongo umri ukaenda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic