November 22, 2019

YANGA leo imebeba pointi tatu muhimu mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Uhuru.

David Molinga ndiye aliyefunga bao lake la ushindi leo uwanja wa Uhuru kwa mpira wa adhabu uliozama jumla ndani ya lango.

Huu ni mchezo wa sita kwa Yanga na mchezo wa pili kwa kaimu kocha mkuu Boniface Mkwasa kuongoza na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Ngoma ilianza kuwa ngumu kwa JKT Tanzania kipindi cha kwanza baada ya Yanga kuandika bao la kwanza kupitia kwa Patrick Sibomana dakika ya 11 na ilisawazishwa dakika ya 13 na Adam Adam dakika ya 13.

Mambo yalizidi kuwa magumu kwa JKT Tanzania baada ya bao la pili kupachikwa dakika ya 22 na Juma Balinya kabla ya David Molinga kufunga bao la tatu kwa mpira uliokufa kwa JKT Tanzania dakika ya 35 na  Danny Lyanga alifunga bao la pili dakika ya 45.

Kipindi cha pili timu zote zilicheza ka hesabu kali na hakuna timu iliyoona lango la mwenzao na kuifanya Yanga kuibuka na ushindi wa jumla ya pointi tatu mazima mbele ya JKT Tanzania.

Aliyeibeba Yanga leo ni Deus Kaseke ambaye alitoa pasi zote za mabao kwa Balinya na Sibomana.  

3 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwalimu Mkwassa anasema anatoa mapumziko ya siku 3 kwa maoni yangu hayo mapumziko ni mengi mno....mimi nilifikiri kwakuwa wachezaji wa timu ya Taifa wamerudi wangeendelea kujumuika na wenzao ili kuanza kuelewana mfumo wa timu kupitia benchi jipya la ufundi....wachezaji wanapunguza stamina ya kucheza kwa dakika 90 pindi unapowapa mapumziko marefu...utakubaliana na mimi kuwa wengi wanakuwa wazito pindi wanapotoka kwenye break...kwa hiyo Mwalimu angeendelea kuwaunganisha kwa kuwapa mazoezi kwani na hizi mvua zinazoendelea kuna wasiwasi kuwa huko mbele timu ikashindwa kukutana na kufanya mazoezi ya pamoja....wakati ni huu kuendelea kutoa dozi mfululizo bila kupumzika pumzika...

      Delete
    2. mwache ajifanye ana huruma sana. atamfuata zahera

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic