MECKY
Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa watapambana kesho mbele ya Azam
FC ili kufuta uteja na Azam FC ambao msimu uliopita waliipiga nje ndani.
Kesho Azam
FC inayonolewa na Mromania, Arstica Cioaba itaikaribisha Kagera Sugar kwenye
mchezo wa ligi utakaochezwa uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:00 usiku.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa maandalizi ya kikosi yapo sawa na wanatambua
ubora wa wapinzani wao jambo linalowafanya wajiamini.
“Tunatambua
kwamba tutacheza na timu ya aina gani jambo ambalo linatufanya tuamini kwamba
tutapata matokeo chanya, hesabu kubwa ni kushinda kisha mengine tutazungumza
baadaye,” amesema.
Mchezo wa
kesho utakuwa wa pili kwa Cioaba ambaye ni kocha mpya aliyerithi mikoba ya
Etienne Ndayiragije ambaye kwa sasa amepewa majukumu ya kuinoa timu ya Taifa
Stars.
0 COMMENTS:
Post a Comment