JUMA
Pondamali, kocha wa zamani wa makipa ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa kwa
sasa yupo tayari kufundisha timu ambayo inamhitaji kutokana na uzoefu alionao.
Pondamali
alikuwa mwalimu wa Beno Kakolanya ambaye kwa sasa yupo Simba pamoja na Klaus
Kindoki kipenzi cha Zahera ambaye amerejea nchini Congo.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Pondamali amesema kuwa alijipa likizo ya muda na sasa muda wake
umekamilika kilichobaki ni kurejea uwanjani akiwa na akili mpya zitakazosaidia
timu kufanya vizuri.
“Natambua
mbinu zote za kumfanya mlinda mlango awe kwenye ubora wake mpaka wachezaji wa
ndani kwani nimewahi kuifundisha timu nikiwa kocha nilipokuwa Lindi najua mbinu
zote.
“Timu ambayo
inahitaji kocha wa makipa nipo tayari kufanya majaribio hata kwa muda wa wiki
mbili wenyewe watakubali kazi yangu na kunipa mkataba,” amesema Pondamali
ambaye kwa sasa amegeukia masuala ya muziki.
0 COMMENTS:
Post a Comment