November 22, 2019

2 COMMENTS:

  1. WANAYANGA PATENI MAJIBU AMBAYO NI HAKI YENU KWA HAYA YAFUATAYO
    🔛Ningependa Kuwashauri Wanayanga Kuulizia Na Kufahamu Mambo Yafuatayo Ambayo Bado Yanautata....Ambayo Wengi Hawajapata Majibu Yanayoridhisha Na Yasipopatikana Yanaweza "Kuchafua Hali Ya Hewa" Pale Mtaa Wa Twiga & Jangwani.
    ⛔ Kocha Mkuu & Benchi La Ufundi Lililo Bora Na La Kisasa
    Baada Ya Kuondolewa Na Kuvunjiwa Mkataba Mwalimu Mwinyi Zahera Na Msaidizi Wake Noeli Mwandila Na Benchi Lote Ka Ufundi...Liliundwa Benchi La Muda Likiongozwa Na Charles Boniface Mkwassa Akisaidiana Na Saidi Maulidi SMG.....Hawa Waliambiwa Wanashikilia Timu Kwa Wiki 2 Wakati Ambapo Kocha Wa Kudumu Anatafutwa.
    Ukiangalia Ligi Kuu Ilivyo...Na Malengo Ya Klabu Kuchukua Ubingwa....Lazima Apatikane Kocha Mkuu Mwenye Kiwango Zaidi Ya Mkwassa Kwani Kulikuwa Hakuna Haja Ya Kumfukuza Zahera Ikiwa Hawakuweza Kumpata Mwalimu Mwenye Uwezo Wa Juu Zaidi Ya Mkwassa....Bado Ili Timu Ishindane Kwa Ubora Na Uimara Katika Kiuchezaji Na Timu Kama Simba Au Azam Lazima Kocha Wa Kudumu Awe Anatokea Katika Nchi Zilizo Na Uwezo Na Utaalamu Wa Kufundisha Soka Zaidi Ya Walimu Wanatokea Ukanda Huu Wa Afrika (Mashariki, Kati, Kusini Na Magharibi)
    ⛔ Ushauri Kuhusu Kocha
    Kocha Wanaotokea Serbia, Yugoslavia, Scotland, Amerika Kusini Ama Ulaya Magharibi Watafaa Kuifundisha Yanga Kwani Timu Inatakiwa Iimarike Kiuchezaji Na Kifalsafa
    ⛔ Ushauri Kuhusu Kocha wa Kudumu Yanga
    Naomba ieleweke, Sikatai uwezo wa makocha wazawa ila wanapungukiwa na Mbinu na kujiongeza katika falsafa mpya za soka la kisasa na mabadiliko yanayofanyika duniani katika taaluma yao ya Ukocha...hapo ndipo wanapozidiwa, wangekuwa wamejiongeza kielimu na kimasomo hili lisingezua mjadala lakini tafiti nyingi na Uzoefu unaonyesha mapungufu hayo na ndio maana klabu zinatafuta makocha wanaotoka nje ambao wamewazidi wazawa katika mbinu za kisasa na katika falsafa mpya ya soka inayobadilika haraka katika karne ya 21
    ⛔ Kuacha Visingizio Vya Ukosefu Wa Pesa
    Kuna Dhana Inayojengeka Kuwa Timu Haina Fedha Kwa Hiyo Tuiishie Kufundishwa Na Wazawa Ambao Uwezo Wao Ni Wa Kawaida Hii Ni Dhana Potofu Ambayo Haina Ukweli Wowote. Yanga Ni Timu Kubwa Ambayo Ina Udhamini Wa Makampuni Zaidi Ya 4 (SportPesa, Taifa Gas, GSM, Maji Ya Afya, Azam Media) Pamoja Na Vodacom....Pili Yanga Ina Wanachama Na Mashabiki Wenye Uwezo Mkubwa Wa Kifedha Wanaojitolea Kuilipia Gharama Kubwa Kubwa Mifano Mingi Ipo Kudhihirisha Hili Kama Ambavyo Ilivyofanyika Huko Nyuma. Isitoshe, Kuendana Na Ukubwa Wa Jina La Yanga Na Msukumo Unaotokana Na Uwekezaji Uliofanyika Simba Itakuwa Ni Aibu Kwa Yanga Kutoingia Kwenye Mabadiliko Ya Kiundeshaji Na Kupata Mwekezaji Ama Wawekezaji/ Ambao Wana Uwezo Kuzidi Hata Huyo Aliyepo Simba...
    ⛔ Uwanja Wa Kaunda Na Kigamboni
    Kumekuwa Na Kusuasua Na Mwendo Wa Kinyonga Katika Utekelezaji Wa Ukarabati Na Ujenzi Wa Uwanja Wa Mazoezi Wa Yanga. Wapenzi Na Mashabiki Wanahoji Hili Na Hasa Wanapoona Wenzao Mtaa Wa Pili Wao Wamekamilisha Uwanja Wao...Ila Yanga Zimebaki Porojo Na Siasa Tu....ILI LAZIMA LIISHE WANAYANGA WAMECHOKA WANATAKA VITENDO

    🚫 Maswali
    ✔ Kwanini Kuna Kusuasua Na Kujivutavuta Kuingia Katika Uwekezaji Na Mabadiliko Katika Yanga Huku Kukiwa Na Kushindwa Kwa Kamati Lukuki Zilizoteuliwa Kuleta Mabadiliko Au Kufanya Vitendo Vinavyoonekana?
    ✔ Je, Viongozi Wana Nia Ya Dhati Ya Kuiinua Yanga Kiuchumi? Kama Wanayo Mbona Mchakato Wa Mabadiliko Unachelewa?
    ✔ Je, Kama Hauchelewi Na Kama Haurakishwi Kwanini Kuna Kilio Cha Ukata Wa Fedha Na Kutaka "KUENDESHA MAMBO KIZAMANI KWA MFUMO WA KARNE YA 19 WAKATI TUPO KARNE YA 21???? Mpira Ni Pesa Na Matokeo Mazuri Na Uendeshaji Wa Timu Kwamaana Ya Benchi La Bora La Ufundi, Miundo Mbinu Bora, Kambi Na Huduma Za Wachezaji Bora Hutokana Na Uwekezaji Wa Pesa....Kwani Uongozi Uliochaguliwa Ulisema Ndani Ya Miezi 3 Hadi 6 Wataiingiza Yanga Katika Mabadiliko Hili Mbona Unasuasua???

    🚫 Wenu Katika Kutoa Ushauri Chanya Kwa Ajili Ya Maendeleo Ya Mpira Tanzania!

    Ahsanteni

    ReplyDelete
  2. Umeeleweka na wenye akili tumekupata vizuri Sana hakika wewe Ni miongoni mwa watu wenye mapenzi mema na club ya Yanga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic