November 1, 2019


Kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya Pyramids FC huko Misri, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema wamejiandaa vizuri.

Kauli hiyo imekuja ambapo hivi sasa Yanga tayari wameshatua Misri kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itakuwa ya kupindua matokeo kufuatia kupoteza kwa mabao 2-1 hapa nyumbani.

Mwakalebela ambaye tayari kashatua Misri mapema kabisa kwa ajili ya maandalizi ya kuipokea timu, ameeleza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na watapambana kupata matokeo.

Ameeleza wana matumaini ya ushindi baada ya kugundua kuwa huko Misri Pyramds inazungumziwa kama timu ya kawaida suala ambalo amelisema linawapa nguvu.

"Unajua hapa Misri Pyramids wanaisema kuwa ni timu ya kawaida kabisa, hivyo inatupa nguvu kuelekea mechi ya marudiano, naimani tutafanya vizuri ikiwemo kupindua matokeo," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Kama ni kweli haya yalioandikwa ni yako bro mwaka basi tutegemee kupoteza tena,timu ya kawaida kwao inakupapasa kwenye uwanja wa kwako ukienda kwao itakuwaje embu tuache kupeana maneno ya faraja

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama kwako inakupapasa basi kwao itakugegeda!

      Delete
  2. Hiyo sio timu ya kawaida hata kidogo na ingelikuwa ni hivo basi wangelichapwa hapa nyumbani angalau mbili Kwa moja.Hapa ulikuwa mteremko lakini Huko kwao ni kupanda kilima. Simba ilipokwenda Huko si matokeo ni marano

    ReplyDelete
  3. Mwakalebela mgumu kuelewa, wenzio wanasema ni timu ya kawaida wakiifananisha na Al ahly, Zamalek, n.k. sisi huku tutasema Namungo ni ya kawaida tukifananisha na uwezo wa Azam, Yanga, Simba n.k

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic