LEO Uwanja
wa Uhuru utachezwa mchezo kati ya Simba na Tanzania Prisons zitakuwa kazini ikiwa ni mchezo
wao wa kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo tangu Prisons ilipopanda daraja msimu
wa 2011 ilipokuwa chini ya Kocha Mkuu Stephen Matata.
Mechi ya leo
inatarajiwa kuwa ya ushindani kutokana na rekodi ambazo zimewekwa na wapinzani
wa Simba, Prisons baada ya kucheza mechi 9 haijapoteza mchezo hata mmoja tofauti na
wapinzani wao Simba ambao wamecheza mechi 8 na kupoteza mmoja mbele ya Mwadui
FC.
Prisons
inahaha kusaka rekodi mpya mbele ya Simba leo ambapo haijawahi kupata ushindi
ikiwa ugenini tangu ilipopanda daraja msimu wa 2011, rekodi zo zipo hivi:-
Mechi zao kiujumla
Timu hizi
zimekutana mara 14 huku Simba ikishinda mara 10, Tanzania Prisons imeshinda
mechi mbili pekee na zote uwanja wa Sokoine huku zikitoa sare mbili.
Idadi ya mabao
Kwenye jumla
ya mechi hizo 14 jumla ya mabao 25 yamefungwa huku Simba ikifunga jumla ya
mabao 20 na Tanzania Prisons ikifunga mabao matano pekee.
Hattrick
Mechi moja
ilileta mabao mengi zaidi ilichezwa uwanja wa Uhuru na Simba ilishinda kwa
mabao 5-0 msimu wa 2014/15 uwanja wa
Taifa na ilipatikana hattrick moja iliyofungwa na Ibrahim Ajibu.
Kadi nyekundu
Kwa upande
wa kadi ni Simba pekee iliwahi kuonyeshwa kadi nyekundu kupitia kwa mchezaji
wao Amir Maftah aliyemchezea rafu Khalid Fupi dakika ya 81 msimu wa 2012/13.
Nafasi zao kwa sasa
Simba
inaongoza ligi ikiwa imecheza mechi 8 na imepoteza mechi moja mbele ya Mwadui
FC ina jumla ya pointi 21 huku Tanzania Prisons ikiwa imecheza mechi 9
haijapoteza mchezo hata mmoja imeshinda mechi tatu na ina sare sita ikiwa na
pointi 15 nafasi ya tano.
Matokeo yao yapo namna hii:
2012-13, Simba 2-1 Prisons uwanja wa
Taifa, Prison 0-1 Simba uwanja wa
Sokoine, 2013-14, Simba 1-0 Prisons uwanja wa Taifa, Prisons
0-0 Simba uwanja wa Sokoine, 2014-15, Prisons
1-1 Simba uwanja wa Sokoine, Simba 5-0 Prisons uwanja wa Taifa.
2015-16, Prisons
1-0 Simba uwanja wa Sokoine, Simba 1-0
Prisons uwanja wa Taifa, 2016-17, Prisons
2-1 Simba, uwanja wa Sokoine, Simba 3-0
Prisons uwanja wa Taifa, 2017-18, Prisons
0-1 Simba uwanja wa Sokoine, Simba 2-0
Prisons uwanja wa Taifa, 2018-19, Simba 1-0 Prisons uwanja wa Taifa, Prisons 0-1 Simba uwanja wa Sokoine.
0 COMMENTS:
Post a Comment