WAWILI WAVULIWA NGUO YANGA
Siri imeibuka. Ni kauli ambayo inaweza kutumika kutokana na aliyekuwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kumvua unahodha wakati huo Kelvin Yondani kisha kumkabidhi Ibrahim Ajibu.
Zahera amefunguka hayo baada ya kutemwa na Yanga juu ya kibarua cha ukocha akiwa ametimiza takribani mwaka mmoja na nusu tangu aanze kazi ndani ya klabu hiyo.
Kocha huyo ambaye ni raia wa Congo, amesema alimvua Yondani sababu ya kuchelewa mazoezini jambo ambalo lilionesha si kiongozi.
"Nilimvua Yondani unahodha sababu ya utovu wa nidhamu, siwezi kuwa na nahodha ambaye anachelewa mazoezini, na wachezaji wenzake walisema hiyo ni tabia yake."
Aidha, kwa upande mwingine aliamua kumpa unahodha aliyekuwa mchezaji wa Yanga na sasa Simba, Ibrahim Ajibu na kumvua tena wiki kadhaa mbeleni.
Zahera ameeleza wakati anampa kitambaa Ajibu alikuwa mtulivu na alibadilika lakini baadaye akawa na nidhamu tofauti tena ndipo alipoamua kufanya maamuzi ya kumnyang'anya pia kitambaa kisha kumpa Papy Tshishimbi.
0 COMMENTS:
Post a Comment