PATRICK Sibomana nyota wa Yanga leo ameibuka shujaa kwa kufunga bao moja la ushindi kwa Yanga mbele ya Ndanda kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa uwanja wa Nagwanda Sijaona.
Yanga ikiwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Boniface Mkwasa imepata ushindi huo ikiwa na kocha msaidizi Said Maulid.
Yanga iliwalazimu wasubiri mpaka dakika ya 75 kushinda mchezo wa leo baada ya kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu bila kufungana.
Patrick Sibomana alipachika bao hilo kwa mpira wa adhabu akiwa nje kidogo ya 18 ambao ulizama jumla ndani ya nyavu za lango la Ndanda FC.
Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 10 ikiwa imecheza mechi tano imeshinda mbili na imetoa sare tatu na kupoteza mchezo mmoja mbele ya Ruvu Shooting.
Wewe muandishi muongoo yanga kashinda mechi tatu
ReplyDeleteDroo moja kapoteza moja Tu
Hizo takwimu umezitoa wapi?
Mwamdish hayuko makin
DeleteHizo hesabu za mwandishi. Wameshinda michezo miwili (yaani hapo wamepata pointi 6), kisha wakatoka sare tatu (ambapo watakuwa wamepata pointi 3). Jumla ina maana Yanga wana pointi 9, tofauti na yeye mwenyewe mwandishi alivyoandika. Hivi atakuwa ameandika kwa ushabiki au anazo records za michezo yote?
ReplyDelete