ZAHERA AUPIGA CHINI UONGOZI WA SASA YANGA
Aliyekuwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ni kama ameupiga chini uongozi wa sasa kutokana na kuingilia baadhi ya mpango yake wakati akiwa ndani ya timu hiyo.
Kocha huyo ameeleza kuwa uongozi huo chini ya Mwenyekiti Mshindo Msolla umekuwa na changamoto nyingi tofauti na mwaka jana ambapo kulikuwa na viongozi kadhaa.
"Nimefanya kazi na viongozi tofauti Yanga ila viongozi wa mwaka jana hawakuwa na uwezo sana, wao wenyewe waliona hawana nguvu kufuatana na hali walikuwa nayo, kazi ilifanyika vizuri sana sababu tulitumika bila pressure '
"Hapa tofauti sasa viongozi hali imebadilika na viongozi hawa ambao wapya wanatafuta sana kujiingiza sana kwenye mambo ya mpira.
"Hata kama ulikuwa Mwenyekiti au Mwalimu idea yako sio idea ya dunia nzima ya makocha wote wote wa duniani haiwezekani Mwenyekiti anakuja anasema unaona Feisal Salum wewe usipande wakati wewe unapanda Makame baki"
Wakati mie kama kocha nawaruhusu wachezaji wangu wa midfield wote wafanye attack, sasa wachezaji wanakuja lalamika kocha mbona Mwenyekiti anatuambia tufanye hivi sasa hapo tunakuwa tunaingiza vitu viwili tofauti'
"Msimu wa mwaka jana nilifanya vizuri na uongozi uliopita kwa kuwa wale walikuwa hawajiingizi na chochote na mambo ya mpira na tulifanya vizuri," amesema Mwinyi Zahera.
0 COMMENTS:
Post a Comment