November 7, 2019


Baada ya kuondoshwa kibaruani na uongozi wa Yanga kama Kocha, Mwinyi Zahera amezidi kuibua madudu ndani ya klabu hiyo kwa kutaja baadhi ya changamoto alizokutana nazo.

Moja ya hizo ni kuhusiana na kambi waliyoweka Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids kuwa hawakufikia kwenye hotel nzuri.

"Kule Mwanza wakati tunajiandaa kucheza na Pyramids viongozi walituweka kwenye hotel ya kwenye mtaa kama wa Kariakoo.

"Ilinibidi niombe namba ya bosi wa GSM ambaye alikuwa Dubai nikazungumza naye na kumueleza juu ya sehemu tuliyofikia.

Bosi akaniuliza kweli Coach mmefikia hapo? Kesho yake akatusaidia tukahama hotel na kwenda hotel nzuri. Namshukuru sana Boss wa GSM".

4 COMMENTS:

  1. Utaongea mengi lakini ndio hivyo kibarua kimeshaota nyasi

    ReplyDelete
  2. We tumeshakuzoea tuachie timu yetu ili turudi kwenye ushindani.

    ReplyDelete
  3. tegemeeni na kipigo toka kwa mnyama januari bila kusahau mnamtafutia kukuza ugonjwa Mkwasa maana mmesahau nini kilitokea mpaka akajiuzulu.
    Baada ya Zahera naona Uongozi ukimfuata

    ReplyDelete
  4. Kwa mtazamo wangu matokeo ya Yanga Ligi Kuu sio mabaya kiasi cha kumfukuzisha kocha maana Yanga imecheza mechi nne, imeshinda mbili, sare moja na kupoteza moja. Upande wa mashindano ya kimataifa ukiondoa ukweli kwamba kufungwa ni sehemu ya mchezo, Yanga imefungwa na timu bora.

    Kama Yanga ikishinda mechi zilizopo mkononi itafikikisha alama 19 amazo ni alama 2 tu kutoka kwa timu inayoongoza.

    Shida kubwa ya Zahera niliyoiona ni uropokaji/kauli zake maana hajui wakati na mahala gani aseme nini.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic