ZAHERA AWABADILIKA WAARABU
Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amesema kuwa anaamini kuwa bado timu yake ina nafasi ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho huku akiahidi kubadili fomesheni katika mchezo wao dhidi ya Pyramids FC ya Misri.
Yanga inatarajiwa kuvaana na Pyramids kesho katika mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuwa mgumu kwa pande zote baada ya mechi ya awali iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kumalizika kwa Yanga kufungwa mabao 2-1, hivyo wanatakiwa kushinda mabao 2-0 ili wasonge mbele.
Timu hiyo tayari ipo Misri tangu juzi iliposafiri ikiwa na msafara wa wachezaji 20 pekee pamoja na viongozi watano wa benchi la ufundi.
Zahera alisema kuwa kama wachezaji wake watacheza kwa kufuata maelekezo yake aliyowapa mazoezini kwa siku nne walizofanya, basi Wanayanga watarajie ushindi.
Zahera alisema kuwa katika mchezo uliopita uliopigwa CCM Kirumba, umakini mdogo wa wachezaji wake ndiyo uliwagharimu na kupoteza pambano hilo la nyumbani, hivyo katika mchezo wa marudiano watatumia mbinu za kushambulia zaidi kama walivyofanya kipindi cha pili walipocheza nyumbani.
Aliongeza kuwa kama walifanikiwa kufunga bao moja nyumbani, basi wana uwezo pia wa kufunga ugenini baada ya kuiboresha safu yake ya ushambuliaji ambayo amemuongeza mshambuliaji Mnyarwanda, Issa Bigirimana ‘Walcott’.
“Hakuna kitakachoshindikana kwetu kama wachezaji wetu watacheza kwa kufuata maelekezo tuliyopeana mazoezini.
“Kama wakifuata maelekezo yangu vizuri, basi tuna uwezo wa kufunga zaidi ya mabao mawili ugenini na hilo linawezekana kwani tayari nimewapa mbinu, mfumo na aina ipi ya uchezaji tuitumie ili tupate matokeo mazuri. “Ukiangalia mchezo wa kwanza tulifungwa kwa bahati mbaya.
Bao la pili walilotufunga lilitokana na sisi wenyewe kukosa umakini baada ya Ngassa (Mrisho) kuuacha mpira akifikiri umetoka kumbe ulikuwa bado na wapinzani kwenda kutufunga.
“Tutabadili mbinu na mfumo tuliotumia kwenye mchezo wa kwanza ni baada ya kuziona hazijafanikiwa, tunafahamu wapinzani wetu wameshazijua, hivyo ni lazima tubadilike katika mchezo wa marudiano.
“Katika mchezo huo tunahitaji kufunga mabao siyo chini ya mawili, tutatumia mbinu ya kushambulia zaidi kama tulivyofanya kipindi cha pili tulipocheza nao CCM Kirumba,” alisema Zahera.
Mnunulieni kaptura zingine huyo mcheza bolingo anae wapiga pesa anawajazia wacheza shoo subirini kesho waarabu wapakate kesho
ReplyDelete