IMEELEZWA kuwa uongozi wa Yanga kwa sasa unahaha kuipata saini ya nyota wao wa zamani Haruna Niyonzima ambaye alikipiga Simba msimu uliopita kabla ya kutimka mazima baada ya mkataba wake kuisha.
Niyonzima akiwa na Yanga alicheza kwa mafanikio makubwa na alikuwa ni kipenzi cha mashabiki kabla ya kuondoka na kuibukia Simba.
Yanga iliyo chini ya Boniface Mkwasa imeanza kusuka mipango mipya kwa ajili ya kikosi cha ushindani na tayari imefika hatua nzuri ya kuinasa saini ya nyota huyo raia wa Rwanda.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mpango wa kusuka kikosi upo na Niyonzima ni miongoni mwa wachezaji wanaowahitaji.
"Tupo kwenye mchakato wa kusuka kikosi upya na kuna watu ambao watakwenda Rwanda kutazama uwezo wa kiungo huyo kabla ya kumalizana naye," amesema.







0 COMMENTS:
Post a Comment