December 6, 2019


Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa ‘Master’ amekiri kikosi chake kuwa na upungufu huku akiahidi kukifanyia maboresho kwa kusajili wachezaji wenye hadhi na uwezo wa kuichezea timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara na KMC uliochezwa juzi Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Yanga imepanga kuifanyia maboresho safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na David Molinga ‘Falcao’, Juma Balinya, Maybin Kalengo, Issa Bigirimana na Sadney Urikhob.

Mkwasa alisema kuwa hakuna ubishi kikosi chao kinahitaji maboresho makubwa, kati ya hayo ni lazima waifumue safu ya ushambuliaji kwa kuleta wengine wapya wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao.

Mkwasa alisema kuwa timu yake imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi lakini umaliziaji ni tatizo, hivyo ni lazima wasajiliwe washambuliaji wengine wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao huku straika rasta wa Biashara United, Mnigeria Innocent Edwin aliyewahi kuwafunga Simba msimu uliopita akikaribia kukamilisha usajili wake Jangwani.

“Lipo wazi kabisa ni lazima Yanga tufanye usajili katika dirisha utakaoendana na timu yetu na kikubwa tunataka kuona tunafanya marekebisho kwenye kila sehemu itakayokuwa na upungufu ikiwemo hiyo ya ushambuliaji ambayo ndiyo yenye matatizo.

“Hilo limeonekana katika michezo ya ligi iliyopita timu imetengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umaliziaji ni tatizo kutokana na umakini mdogo wa washambuliaji tulionao katika timu,” alisema Mkwasa.

1 COMMENTS:

  1. Mkwasa asiwe mbinafsi kiasi hicho, aseme wazi kwamba moja ya matatizo yaliyopo Yanga ni pamoja na uwezo mdogo wa benchi la ufundi; makocha.
    Katika mechi ya KMC, Yanga ilikosa ushindi kwa mapungufu au uwezo duni wa benchi la ufundi, hususan Kocha Mkwasa.
    1. Alipanga timu kama iliyocheza na Alliance bila kuhali utofauti na mbinu na mazingira ya mechi.
    2. Timu ilizidiwa kwenye kiungo na hatimaye mashamhulizi, kocha hakufanya mabadiliko ya kimfumo na mbinu, akiwaacha mabeki wake kuchishwa, hadi dakika ya 70; kipindi cha pili
    3.Beki Jafari na Lamine, walifanya makosa mengi na mwishoni walielekea kuelemewa na wapinzani wao, kocha akapotezea
    5.Kocha aliamua kumuingiza Said Makapu dakika ya 94, baada ya KMC kusawazisha
    6. Yondani na Lamine walifanya makoss zaidi ya 6, shukurani tu ni kwa umakini mdogo wa washambuliaji wa KMC
    Kwa kifupi kidole chake kisielekee kwa wachezaji tu, tatizo ni kubwa zaidi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic