December 22, 2019


MLINDA mlango wa Tanzania, David Kissu anayekipiga ndani ya kikosi cha Gormahia kwa sasa amesema kuwa mshambuliaji Yikpe Gnamien, 'mwili jumba' ambaye yupo Bongo kumalizana na Yanga kwa sasa sio mchezaji wa kawaida kutokana na aina ya magoli anayofunga.

Kissu ambaye amewahi kuwa mlinda mlango wa zamani wa Simba na Njombe Mji ambaye kabla ya kuibukia Gormahia alikuwa akikipiga Singida United amesema kuwa anamtambua vema Gnamien wapinzani wa Yanga watapata tabu.

"Ni mshambuliaji makini anayefunga mabao kwa namna zote ndani ya uwanja kwa kichwa, miguu mpaka anakera kwa usumbufu akiwa ndani ya uwanja.

"Moja ya bao lake matata ilikuwa ni kwenye mechi yetu dhidi ya AFC Lopards wakati tukishinda kwa mabao 4-1, Novemba 10 alifunga kwa kichwa kwa ustadi mkubwa hivyo ana nafasi ya kufanya makubwa akipewa nafasi," amesema.

Yanga imeshamalizana na nyota wa nne sasa ambao ni Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima, Tariq Seif na Lamine Moro na ipo kwenye mazungumzo na raia huyo wa Ivory Coast ambaye amevunja mkataba na timu yake.

3 COMMENTS:

  1. ngoja tuone maana manenotu bila hata vitendo haisaidii

    ReplyDelete
  2. Mbona ni mechi hiyo tu aliyofunga. Msikuze mambo, alikocheza msimu mzima amefunga goli nane. Timu aliyotoka kuja Gor alikuwa amefunga matano

    ReplyDelete
  3. Balinya tuliambiwa hivyo hivyo. Mfungaji bora ligi ya Uganda kilichotokea tunakijua.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic