HIVI NDIVYO KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA SIMBA KITAKAVYOPANGWA, NI BALAA TUPU
Wanachokifanya sasa mabosi wa Yanga ni kushusha mashine maalum ambazo zitawasaidia katika msimu huu wa 2019/20 lakini zaidi ni juu ya mechi yao dhidi ya Simba ya Januari 4, mwakani.
Vibopa hao wa Yanga kwa sasa wanachokifanya ni kudondosha sura mpya katika dirisha hili dogo la usajili ambazo zitawapa nguvu katika mechi hiyo ya wapinzani wao licha ya awali Yanga kuonekana kuwa dhaifu dhidi ya wapinzani wao hao.
Hadi sasa Yanga wameshusha nondo tatu katika dirisha hili dogo la usajili lililofunguliwa Desemba 16 ambazo ni washambuliaji Ditram Nchimbi na Tariq Seif huku pia wakimjumuisha beki Adeyum Saleh.
Tariq ametua klabuni hapo akitokea Dekernes FC ya Misri, wakati Nchimbi ametua akitokea Azam FC na Adeyum akitoka kwa ‘wajeda’ JKT Tanzania.
Kabla ya kukutana na Simba, Yanga pia watashusha sura mpya ambapo wapo katika hatua za mwisho za kuwasajili kiungo mchezeshaji wa AS Kigali, Haruna Niyonzima na winga wa UD do Songo, Luís Jose Miquisson.
Baada ya usajili huo wote kukamilika Yanga watakuwa na kikosi ‘chuma’ ambapo katika mchezo huo na Simba wanaweza kukipanga kwa namna hii.
Farouk Shikalo ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuanza langoni mwa timu hiyo ya Yanga kutokana na takwimu kuonyesha ndiye amecheza mechi nyingi za ligi kuliko wenzake ambao ni Metacha Mnata na Ramadhani Kabwili.
Kwa upande wa beki wa kulia, Juma Abdul ambaye aliitwa katika timu ya taifa ya Tanzania, Kilimanjaro Stars iliyoshiriki michuano ya Cecafa huku mashine mpya Adeyum Saleh ndiye anayepewa nafasi ya kuanza beki wa kushoto.
Mabeki wa kati watasimama Kelvin Yondani na Lamine Moro ambaye Jumatatu hii alilipwa mishahara yake aliyokuwa anaidai klabu hiyo.
Kwenye eneo la viungo, Papy Tshishimbi ambaye tangu kuingia kwa kocha Charles Mkwasa anachezeshwa kama kiungo mkabaji, ndiye ataanza eneo hilo akishirikiana na Niyonzima ambaye muda wowote atadondoka Dar kuungana na wenzake.
Mnyarwanda Patrick Sibomana, katika kikosi hiki anatarajiwa kupangwa kama winga wa kulia wakati Luís Jose Miquisson aliyetoka UD do Songo akipewa nafasi ya kucheza kama winga wa kushoto.
Mastraika wapya Nchimbi na Seif ndiyo ambao wataanza katika eneo hilo la ushambuliaji ambapo pia anaweza kucheza David Molinga na mmoja kati yao.
Kwenye kikosi hicho Metacha, Paul Godfrey ‘Boxer’ aliyerudi baada ya kupona majeraha, Ally Mtoni ‘Sonso’, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Abdulaziz Makame na Balama Mapinduzi wenyewe wakitarajiwa kuwa wachezaji wa akiba.
Umetaja kikosi kitakachoikabili simba . Acha nami nikutajie fowardi ya simba itakayo ihenyesha defensi ya yanga . winga ya kulia ni mfumba jicho , namba tisa kati ni medie kagere , namba kumi nyuma ya mshambuliaji wa kati ni MK14 , mshambuliaji kutokea winga ya kushoto ni Nguvu ya mamba kumai. wengine siwataji ili nisiwatie hofu
ReplyDeletehahahaha yanga bhana mbona munateseka kwanini mteseke?
ReplyDelete