ILIKUWA
miaka, miezi, wiki na juzi Jumamosi ikafikia ile siku muhimu kwenye soka la
Tanzania, ndiyo, ni Klabu ya Simba kuzindua viwanja vyao viwili vya mazoezi
vilivyopo Bunju jijini Dar. Hongera sana kwao, tunajivunia wao.
Simba ina
miaka zaidi ya 80 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1936 kwa miaka yote haikuwahi
kuwa na uwanja wao wa mazoezi tu, ililazimika kulipia Sh 500,000 kwenye viwanja
vya kukodi ili wachezaji wapata nafasi ya kufanya mazoezi.
Ilikuwa aibu
sana kwao, na walitumia gharama kubwa kulipia fedha kwa ajili ya kufanya
mazoezi tu, lakini pongezi kubwa kwa mfumo waliouchagua ambao leo hii unaleta
matunda.
Simba
iliamua kuingia kwenye uendeshaji klabu kwa mtindo wa hisa, mwekezaji mkuu,
Mohammed Dewji ‘Mo’ alichukua hisa 49% na klabu imebakiwa na 51%, hapa mageuzi
ndipo yalipoanzia.
Baada ya
hapo, Simba wakafanikiwa kurejea kwenye viwango vyao na kurejesha mataji mawili
ya ligi kuu kisha wakafanya kweli kimataifa baada ya kucheza hadi robo fainali
ya Ligi ya Mabingwa Afrika, haya ni mafanikio ya kujiendesha kisasa.
Ukiachana na
hilo, pia wamefanikiwa kujenga viwanja vyao viwili vya mazoezi, kimoja cha
nyasi asilia na kingine cha nyasi bandia, hapa itetegemea na kocha anataka
kufanya mazoezi kwenye uwanjani upi, kongole kwao tena.
Na
ukiangalia hili limewezekana baada ya kuachana na ule mfumo mmoja wa kuongozwa
na wanachama halafu wanachagua mwenyekiti au rais ambaye anakuwa hana malengo
sahihi na klabu.
Tuliona
awali wakati wa mfumo wa uanachama pekee, walipita viongozi kadhaa ndani ya
timu hiyo na kwenya kampeni walitumia maneno matamu ya kuwadanganya wanachama
wao ili wawape kura lakini mwisho wa siku hakukua na maendeleo.
Kila
kiongozi aliyeingia madarakani aliona kama ni kitu kigumu sasa chini ya Mo
Dewji naona hili limewezekana, kumbe kila mtu akiamua inawezekana, tufanye kazi
tuache maneno.
Angalia leo
hii hata wapinzani wao, Yanga nao wameanza mchakato mdogomdogo lakini naona
wazi kama itachukua muda mrefu kukamilisha kile ambacho wamepanga kukifanya hii
ni kutokana na mfumo uliopo.
Wanapaswa
kubadilika, wasione kama wanaiga, ngoja niwaambie, kuiga maendeleo ni kawaida
sana tena mnaweza kufanya vyema zaidi ya wale waliotangulia.
Ni aibu
mpaka leo hii klabu hizi kongwe kuonekana zinashtuka sasa lakini kwa kuwa Simba
wameshafanya tunawapongeza na sasa kazi ihamie kwa Yanga kwani wao pia ni kama
kioo kwa timu zingine kibao zinazochipukia.
Ni aibu kila
siku kukodi viwanja kwa ajili ya mazoezi tu, ni aibu kubwa sana. Yanga ina
mtaji mkubwa, inapaswa kubadilika na kujiendesha kisasa. Mpira wa sasa ni fedha
na hilo halikwepeki.
Kama
utakumbuka kipindi Yanga ipo chini ya mwenyekiti Yusuf Manji ilikuwa na
wachezaji waliowahitaji, fedha kwao haikuwa tatizo kama ilivyo sasa hivi, sasa
Wanajangwani wakubali wakatae wanahitaji mtu wa aina hiyo ili kurejea kwenye
mstari wao. Nitarejea panapo majaaliwa.







Ni muhimu Kumpata muwekezaji mwenye sifa kama sole za Mo ambae ana mapennzi na Simba tangu hapo utotoni na uwezo wa kimali
ReplyDeletesio ambae anatafuta penye lengo la kumtajirisha bila yakuwa na lengo la mapennzi na timu