December 15, 2019


Taarifa ambazo ni za chini ya kapeti zinaeleza kuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha yupo kwenye mchakato wa kumpelekea straika wa Difaa El Jadid ya Morocco, Simon Msuva Benfica ya Ureno.

Taarifa imeeleza kuwa Tiboroha ambaye ni wakala wa mchezaji huyo ambaye aliwahi kuichezea Yanga, atampeleka Msuva Benfica ya Ureno ambao nao watampeleka kwa mkopo wa miezi sita Ugiriki.

Timu inayotajwa kupelekwa kwa Msuva Ugiriki ni Panathinaikos F.C inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Tangu Msuva aelekee Morocco akitokea Yanga, mchezaji huyo amekuwa na mchango mkubwa ndani ya waarabu hao na akiwa tegemo kutokana na kuitendea haki kazi yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic