December 15, 2019


Imeripotiwa kuwa mabosi wa Yanga wameanza kufanya mawasiliano na winga wa kimataifa wa Msumbiji na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Luis José Muquussone.

Yanga wameanza mazungumzo na straika huyo anayecheza kwa mkopo UD Songo ya Msumbiji ili kumsajili katika dirisha dogo la usajili ambalo linafunguliwa Jumatatu ya wiki ijayo.

Muquussone anakumbukwa kwa kuifunga Simba katika mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam, mechi ambayo ilimalizika kwa sare ya 1-1.

Usajili huu wanaupigania Yanga wakiwa wametoka kumalizana na Tariq Seif ambaye alikuwa akikipa huko Misri katika Ligi Daraja la Pili.

3 COMMENTS:

  1. KWANINI YANGA INATAKIWA IFANYE MABADILIKO KUINGIA MFUMO WA UWEKEZAJI NA UENDESHAJI WA KISASA NDANI YA SIKU 60?
    ❇ Kuimarisha Timu na Kikosi kwa ajili ya Kutoa  Ushindani kwenye mashindano mbalimbali inayoshiriki (Usajili wa Wachezaji Bora ndani na nje ya Nchi, Mishahara Bora, Posho, Kambi Bora, Ujenzi wa Miundo Mbinu Bora na Viwanja vya Mazoezi Bora, Tiba na Lishe za Wachezaji, kubadilisha mfumo klabu kuendeshwa kisasa na kisayansi)
    ❇ Klabu kuwa katika mbio za kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu ama FA...ili kupata nafasi ya Kuwakilisha nchi katika mashindano yanayoandaliwa na CAF

    ⛔Sababu zinazokwamisha hayo mawili yasifanyike:
    ❇ Jitihada kutoka kwa Wasio itakia Mema Yanga
    Kuna nguvu kubwa inatumika kutoka kwa maadui wa Yanga (Simba, TFF, Bodi ya Ligi, Mamluki waliopenyezwa kwenye Uongozi Yanga kupitia Kamati zilizoundwa hivi Karibuni, Vyombo Vya Habari, Mitandao ya Habari, Wapenzi wa Yanga wasio waaminifu na wanachama wasio waaminifu wanaorubuniwa)
    ❇ Hawa wanafurahia hali hii iliyopo na mambo yanavyoenda wakiwalisha matango pori wapenzi wenye uchungu na Yanga kwa kuwahadaa na kuwalaghai kuwa mambo ni mazuri tu, wawe na subira vile vile Viongozi waendelee kuwasajili wachezaji wa bei nafuu wasio na sifa za kuichezea Yanga ambao hawana uwezo wa kutoa upinzani uwanjani kwa kuleta ushindi na matokeo chanya. Matokeo yake vyombo vya habari vya mtaani vinaitwa kuzipaisha habari hasi kwa nguvu isiyo ya kawaida!
    ❇ Hawa wangependa Klabu iajiri makocha wa gharama ya chini na kushirikisha wanachama na mashabiki wasio na fikra pevu, endelevu, elimu na uweledi wa hali ya juu kuiendesha klabu...hawa wanafanya hizi fitina za soka kisayansi wakitumia kibwagizo cha wimbo Yanga haina pesa na inashindwa kulipa mishahara ......ukweli ni kuwa dawa ya kupata pesa ni kukaribisha wawekezaji tena haraka na mapema ndani ya siku 60.......
    ❇ Lakini unaposhauri hili la kutafuta njia ya kujikwamua katika hali iliyopo....makundi haya ya watu niliyoyataja hapo juu yanapinga na kutoa sababu ambazo hazina mashiko kwa maslahi yao binafsi...sasa unahoji kama ushabiki wao ni wa dhati ..Je hawa hawaoni uchungu kwa kudhoofika kwa timu? Je, hawa hawataki Yanga ipige hatua ama ni nini? Jibu ni rahisi na haishangazi kuona wanatoa sababu hizi kwakuwa wanatumiwa na klabu ya upande wa pili...na nguvu waliyonayo kiuchumi klabu hiyo ya mtaa wa pili wamesajiliwa kujipenyeza kurubuni makundi hayo niliyoyataja hapo juu ndio sababu hao niliowataja wanatoa kauli hizo...na vyombo vya habari vya mtaani vinaitwa kuzipaisha habari hasi kwa nguvu isiyo ya kawaida!!!...

    ❇ Kama ukichunguza utajua Upande wa pili kwa klabu jirani wanajiapiza kwamba wanauwezo wa kuchukua ubingwa kwa gharama yoyote. Unajiuliza hiki kiburi wamekipata wapi? Je, wanajuaje kama watachukua ubingwa wakati ligi ina mechi 38....na ndio kwanza zimechezwa mechi 13? Labda inawezekana wanasema wana uhakika huo kwasababu ya nguvu ya kiuchumi iliyopo ambayo inatumika kuliimarisha Klabu na pia kuzidhoofisha klabu nyingine zikiwamo hata kuziingilia na kuzirubuni taasisi zinazoendesha soka na timu pinzani aidha kwa njia ya moja kwa moja ama kwa njia za kificho na kisayansi kama ambavyo inafanyika hivi sasa?

    Daima Mbele Nyuma Mwiko!

    Ahsanteni

    ReplyDelete
  2. ivi kwa nini hii page mnapenda kuandika taarifa za kuiga iga ambazo hazina kina wala kuendana mfano mnajua picha mliyoweka ya mchezaji wa mamelod haviendani na taarifa luis wa ud songo hio sio picha yake chukueni taarifa sehemu na mzifanyie uchambizi na nyny kucopy sio shida wala haikatazwi lakini chambueni mjue uhakika wa taarifa lakini sio kuchukua taarifa alaf hamjui meanfull.nna uhakika mwenye plevaledge na hii site hajitambui hata nn anapost.hebu kuweni professional basi fanyeni hata research

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic